Monday, 10 February 2020

USILIE BASI na Joseph C. Ogbu (JoeNwaOgbu)

 Usilie tena, Mama anajua
Futa machozi, utabasamu kama maua
Furaha yako, uchungu wako, yote anafahamu
Usikate tamaa, hata kama moyo umejawa na ugumu.

Jipe moyo, maisha ni zaidi ya maonyesho
Usikate tamaa leo, kwa faida ya kesho
Kaza mshipi, weka malengo
Na Mama anajua, maisha yana wapi pengo.

Mwiba moyoni
Uchungu akilini
Macho yanavimba; Kwa nini haya yote?
Usilie, tulia, Bikira Maria anajua yote. 

Hata kama mwilini baridi kali
Tazama furaha inaguruma, haipo mbali
Ili ombi hewani ni unyenyekevu
Tukae na kusali bila uvivu.

Basi, tabasamu  kidogo
Ili moyo uepuke kuishi na mzigo
Kwa kuwa maisha ni baraka si adhabu
Iliyopangwa na Mungu kuendeshwa kwa utaratibu.

Sasa simama ucheze ngoma ya heshima kwa  furaha
Bila kujali maisha ya kisasa
Na bila kutembea na kucheza kwa hofu
Kwa kuwa furaha pekee, daima yaponya miguu mibovu.

SMILE ON THE FACE; BUT...? by Fr. Joseph C. Ogbu

Imagine! Calmly water turning thicker than blood, Evils gently overflowing like flood. God! be merciful on your precious world, And allow n...