Peke
yako, sitakuacha
Wewe
upendo, sitakuficha.
Upendo
hujenga maisha yawe imara,
Kabisa
kupenda haina hasara.
Nashangaa
tena hauna hata tabaka,
Ila
ndani hujazwa tupu baraka.
Loo!
zawadi kubwa sana tulizojaliwa,
Kugawia
wenye nguvu na waliolemewa;
Sawa
kwa wakubwa na pia kwa wadogo.
Tukijua
upendo una nguvu si kidogo;
Basi
Upendo mikononi tushike sote,
Ili
dunia iendelee kumeremeta kwa wote.
