Wapi unaogelea huu ukoma wangu
Kwako nakimbilia ee Mungu wangu,
Magoti chini; macho kwako
Tutazame usoni; Sisi watoto wako.
Sauti nzuri tena katulisha kwetu sasa,
Lo! kila tabia mbaya, ukoma kabisa
Tuziache na tufuate mazuri kwa unyenyekevu
Ili daima tuishi kwa furaha na utulivu.
Uendelee kukaa nasi ee Mungu Mwema
Wala usisite kutuponya katika kila wetu ukoma
Tuweze tena kukuimbia nyimbo zetu nzuri
Kwa kututendea haya makubwa mazuri.
Ee Mungu Mwenyezi wa milele
Naomba uendelee kutuongoza mbele,
Utuponye jumla bila kubakiza hata kipengele
Maisha yetu yapambwe na amani na vigelegele
Ili nyumba zetu; mfano mzuri huku na kule
Na njia zetu; mafanikio na baraka tele.
…...…..................................................................
....................................................
Wazo lililotengenezwa kutoka kwa maneno ya Baba Abate Pambo Martin Mkorwe OSB, "KWA HUSU UKOMA" ~ 26/11/2021















