Alleluia! ni wimbo wetu; hatuna mashaka,
Cherekochereko, njia yetu; kaja na Pasaka,
Furaha tele, nyoyo zetu; kwetu ni baraka,
Vigelegele safi, ndimi zetu; hatuna haraka,
Tembea kwa maringo, yupo kwetu; Kristo Mfufuka,
Huzuni kwaheri, furaha karibu; Kristo kajitoa sadaka,
Tabasamu basi; Kristo Yuko nasi, hautaanguka,
Basi, naomba nikutakie neema na fanaka
Katika kipindi hiki cha shamrashamra za Pasaka,
Na mema yaendelee kukaa nawe bila mipaka,
Ili daima uishi na kuneemeka,
Na baraka zitiririke kama mvua wakati wa masika.
