Monday, 23 November 2020

UTENZI WANGU KWAKO, na Joseph C. Ogbu (JoeNwaOgbu)

Pokea wangu utenzi
Ee Bikira wetu Mpenzi,
 Malkia wa mbingu na dunia
Sijui neno gani zuri kukusifia,
Hauna doa wala hila 
Mwenye upendo kwa kila kabila,
Wema wako daima hauzuiliwi na mipaka
Uzuri wako kama nyota daima huwaka,
Maisha huoana na yako huruma
Utenzi huimbwa, Umejaa neema,
Kwa moyo safi twakushukuru
Kusafiri nawe haikosekani nuru,
Basi, pokea wangu utenzi
Mama yetu,  Bikira Maria Mpenzi.

SMILE ON THE FACE; BUT...? by Fr. Joseph C. Ogbu

Imagine! Calmly water turning thicker than blood, Evils gently overflowing like flood. God! be merciful on your precious world, And allow n...