Unishike
Mpenzi wangu nifurahi; Kukaa Nawe kabisa si mwiko
Midomo
yangu tu Shukrani; Nikumbukapo Uzuri Wako,
Moyo
wangu unashangilia; Wema Wako nafaidia
Uwepo
Wako nafurahia; Huruma Yako yasaidia,
Kwa
moyo safi nasherekea; Sura Yako nasemea
Wimbo wangu nimekuletea; Ngoma safi imekolea,
Hapa sasa unifundishe; Kukuweka mbele katika kila jambo
Kwa
Neno Lako wala sibishe; Kwa kuwa Wewe ujuaye
yote mambo,
Pamoja
Nawe ni kwangu bahati; Kukaa Nawe ijaayo maisha amani
Uniongoze
nikufuate kwa moyo dhati; Hapa sasa na pote
mahalini,
Na
Uujaze moyo kwa upendo; Ili moyo daima ukose nafasi ya chuki
Najua
njia Yako haina magendo; Na neema Zako zinalinda miguu katika dhiki,
Basi
Eee Mungu Wangu; Uniongoze katika njia zako
Ili
nitimize ulichoweka kwangu; Na mwisho nije salama Kwako.
