Wednesday, 29 September 2021

HEKIMA YA BABA; IDUMU MILELE na Joseph C. Ogbu (JoeNwaOgbu) 28-09-2021

Bora uchukiwe sababu ya wivu
Utokanao na wako mfano bora 
Si kwa sababu kutokujitahidi na uvivu 
Au kuchukia kazi na kulala kila mara.

Simama, vaa mkanda; acha kushika mashavu
Usiogope, kila siku inatujia na yake nguvu
Maisha mazuri sana, kabisa si mabovu
Kazi hazikwepeki; mweke Mungu mbele, bila  ulegevu.

Hekima ya Baba iendelee kudumu milele
Inasikika masikioni bila hata kelele 
Na hu i pa miguu nguvu kusonga mbele 
Na daima huua maovu kama mshale.

…...…..................................................................
....................................................
Wazo lililotengenezwa kutoka kwa maneno ya Baba Askofu Mkuu Geravas M.  Nyaisonga,
28/09/2021

SMILE ON THE FACE; BUT...? by Fr. Joseph C. Ogbu

Imagine! Calmly water turning thicker than blood, Evils gently overflowing like flood. God! be merciful on your precious world, And allow n...