Huzuni kapata umaarufu haraka,
Tanzia! barua likasomeka,
Macho yalitiwa upofu, kwa machozi kutirika,
Alfajiri sana Jeshi kaondoka
Wala adhuhuri hukuweza fika.
Furaha yetu ilipojituliza
Huzuni ikapaaza sauti,
Tamaa yetu tungekuuguza,
Ila haikutuonea huruma mauti,
Utume kweli ungeendeleza,
Basi Kifo naye msaliti.
Loo! Dunia basi
Machozi yetu kasi
Padre tena haupo nasi
Imani umeilinda
Kristo Mauti lishinda
Na huko kwake mekwenda,
Na Kwake umejituliza.
Hakika kifo ni fumbo
Wala hatuelewe lake jambo.
Padre wetu Asterius Mutegeki
Sauti yako tena haisikiki,
Katamani kabisa tucheke
Wazo la uwepo wake,
Ndo kaja Mwenyezi aliyemtaka
Nasi tukabaki na kuchoka.
Katika wema na kheri,
Mpe taji jemadari,
Kwenye udhaifu na shari,
Huruma yako itakabali,
Twaomba astahili,
Umuangaze kwa yako miali,
Astahili rehema zako.
Lala salama Baba,
Usafiri salama Mtu mwema
Naenda salama Mpendwa
Tutakutana kwa Mungu Baba.
