Sauti nzuri iliosikika asubuhi; Ghafla kaenda wapi jioni hii?
Tabasamu hufanya jumuiya ifurahi; Tena hayupo katika jamii,
Wapi yupo sasa wetu Mama; Ulimi unashindwa hata kusema
Nasi ugumu tunapata kusema; Sista wetu safiri salama,
Kifo, uchungu, mioyo imejazwa; Sababu hatupo naye Mpendwa
Uso ulionekana mzima jana; Kwa machozi wote twatafuta Sana,
Mama Kanisa kafiwa na mtoto; Sote tumeguswa kama watoto
Mama KIP, kweli ni pigo zito; Ni Mungu kamchukua wake mtoto,
Wanashirika wa Kilimanjaro poleni; Ni imani, Sista yuko Mbinguni
Sote tukumbuke tuko folenini; Na mwisho tutakutana naye Mbinguni,
Basi, Mungu mwenye huruma; Umjalie Sr. Wenseslaus Olomi neema
Ili aweze kukaa nawe daima; Na afurahie kuwa Nawe vema.
