Malkia wangu, mshupavu sana, mtu mwema,
Uzee
haukujui, sura huvutia, eeh Mama,
Mzuri
wewe, zaidi ya wanawake wote, eeh Mama,
Upo
safi kabisa, huna doa, eeh Mama,
Daima
natamani kukaa nawe, eeh Mama
Kwa
Upendo na Heshima mkubwa, eeh Mama,
Naja
kukuimbia wimbo mzuri, eeh Mama,
Sasa na
mwisho wa dunia, eeh Mama,
Zumari
hapa, makofi kwako, eeh Mama,
Mtu
asiye na dosari, zeze inasema, eeh Mama,
Matari
imechangamka, kuchoka hakuna, eeh Mama,
Kengele
inasikika pote duniani, ni heshima ya Mama,
Umsaidie
Mwana aishi bila kukusahau, eeh Mama,
Maisha
yote tutembee pamoja, eeh Mama,
Ninapopotea
uje hima kunirudisha, eeh Mama,
Kwa
kuwa dunia nzuri, mambo si mepesi, eeh Mama,
Sasa
kwako naleta zawadi zangu, eeh Mama,
Zilizoambatana
na unyenyekevu, eeh Mama,
Naomba
tucheze na tufurahi kama Mwana na Mama, eeh Mama,
Kwa
maisha bila wewe hali tete, eeh Mama,
Na
maisha rahisi si lele-mama, eeh Mama,
Hapa
nipo, nakungojea kwa hamu, eeh Mama,
Sina
kwingine kwa kwenda ila kwako, eeh Mama,
Shela
yako, imepambwa kwa nyota, eeh Mama,
Wewe
pendo langu na furaha yangu, eeh Mama,
Tabasamu
lako huponya kila maradhi, eeh Mama,
Ni wewe
Mwanamke pekee, daima nakutamani, eeh Mama,
Wewe
chaguo langu si Mwingine, eeh Mama,
Joho
lako huvutia moyo wangu, Mama,
Maisha
yanakwenda, furaha tele, eeh Mama,
Ngoma
zinapigwa, roho inarukaruka, eeh Mama,
Safari
ndefu, miguu unaisukuma, eeh Mama,
Filimbi
hewani, tarumbeta zinalia, eeh Mama,
Kinanda
chaimba Nuru usiyefifia, eeh Mama
Haya
yote, Upendo sababu, eeh Mama,
Na
ndiyo masikio yanasikia, marimba yapigwa, eeh Mama,
Ahadi
kwako, Mimi na Wewe, eeh Mama,
Ni kwa
ajili yako, moyo hauonji unyonge, eeh Mama,
Ni Wewe
mama, kila vita, Ushindi Kwako, eeh Mama,
Mpendwa
jasiri, kinanda kinapanda, eeh Mama,
Tucheze
sasa, moyo umekukuta, eeh Mama,
Furaha
yangu na kilio changu uvipokee, eeh Mama,
Nuru
yako, huondoa giza, eeh Mama,
Usiku
na mchana gitaa laita jina, eeh Mama,
Mambo
yote wewe wayajua, eeh Mama,
Ulimi
wangu, hutangaza Upendo wako, eeh Mama,
Na
ikiwa kiangazi ama masika,mimi pamoja nawe, eeh Mama,
Malkia
wangu, Mwombezi wangu, Asante eeh Mama,
Bikira
wangu, Maria Mwema, wewe ni wangu Mama,
Maisha
yote, ombi langu, ni yote mema, eeh Mama,
Ili
Safari ya dunia, daima iambatane na
neema,eeh Mama
Na moyo
daima ukae kumsifu Mwanao, Yesu Mwema, eeh Mama,
Na
mwisho naomba maombezi yako, eeh Mama!

