Swahili

UJIO WA ASKOFU MKUU by Joseph C. Ogbu (JoeNwaOgbu)

Ujio wa Askofu Mkuu ni wasifu mfupi wa Askofu Mkuu Gervas John Mwasikwabhila Nyaisonga wa Jimbo Kuu Katoliki la Mbeya-Tanzania. 
Ni kitabu kilichoandikwa kwa mistari na vina (kisarambe) ikionesha wasifu wa Askofu Mkuu.

*********
Nawashukuru Mafrateri Victor Basilius na Charles Mtuka walioshirikiana nami katika kutafisiri kitabu hiki kwa Kiswahili.

I
Kwa midomo ya shukrani kwako Mungu twafika,
Kwa upendo wako kichwa chaneemeka,
Mwili wako dhidi ya ugonjwa na kifo akufunika,
Siku zaja pamoja na paji ili kukua na kuzeeka,
Usiku na mchana vyakufanya mwenye fadhili hakika,
Kutangazia uimara mioyo iliyopondeka,
Kupitia moyo uliowekwa mamlaka,
Ustadi wa Mungu umeoteshwa na kudhihirika. 
II
Hapa ni wimbo uelezao ukuu na ukweli wa Mtumishi,
Afanyaye kazi kwa umakini asiye mshabiki bali Mtumishi,
Alizaliwa Novemba, mwezi mbarikiwa wa kuishi,
Tarehe tatu, mwaka moja tisa sita sita, wa mema matashi,
Kuvutia dunia siku ya kwanza kwa kilio pako pa kuishi,
Si tu furaha kwa familia hata wapita njia hawakanushi,
Mbozi-Mbeya kulisikika bila wa binadamu ushawishi,
Yote chini ya ulinzi wa Mungu Tarishi. 
III
Safari ya maisha kuwa ya kimungu ilijidhihirisha,
Ni katika mwaka huu tunajikumbusha,
Moja tisa nane mbili na moja tisa nane tisa kisha,
Elimu ya msingi na sekondari kakamilisha,
Kafanya mpango wa kimungu, tulivu, ajabu wa kutafakarisha,
Seminari kuu kuwasili kuwa na moyo na wito haikutosha,
Ni upendo wa Mungu na ufadhili wa Askofu ulimwezesha,
Waliongoza hatua zake mpango kukamilisha,
Ili maisha yasiachane na utakatifu wake wa maisha.
IV
Ndoto zadhirisha ukweli, na sauti za pekee zasikika,
Na midomo vyaimba kwa sauti isiyo linganishika,
Kumkaribisha katika Altare takatifu mtu aliyetukuka,
Bila ya gharama yoyote paji lake ni chapa isiyofutika,
Kurejea tukio la moja tisa tisa sita lile lililosifika,
Ilikuwa Julai kumi na moja tarehe iliyotukuka,
Ni siku ile ya upadirisho kwa Imani alisifika,
Akiwa na nguvu thabiti kutangaza neno na Imani iliyoimarika,
Ikikuza ukweli wa mbingu nakukata kama upanga wa shujaa hakika.
V
Hakika, amesimama siku zote katika utume,
Kihalali alifikia upadre kuonesha wake utume,
Kutoa neema za kibaba kama wakili paroko kiutume,
Atoa furaha na Sakramenti kwa kanisa la kitume,
Huduma yake ya upendo yadhihirisha uzuri wa utume,
Afanya kazi kwa neema na shime,
Kwake ujasiri, haki na amani sehemu ya utume,
Kuwapigania waliokataliwa na kuwapa shime.
VI
Utume umeimarika kwa neema itokayo juu kwa baba,
Si tu kuwa mlezi Seminari bali kuwa Mwalimu na baba,
Na kufanywa Mkufunzi na kuwa kichwa haya si haba,
Mwenye ufahamu na kuwapa ufahamu kama baba,
Kuwafanya wote mwanga wa kweli kubeba.
VII
Aha! Kwa upadre wake waweza kuona ukamilifu,
Wa kibaba ukifunua majukumu yake tukufu
Kisha sikia zumari, filimbi kwa furaha kamilifu,
Bila kuchoka vikiimba, vikicheza na kusifu,
Kwa baraka ya tisa machi kwa Mungu toa utukufu,
Mnamo mbili sifuri moja moja katika Kanisa Katoliki Takatifu,
Huko Dodoma kusimamishwa Mchungaji mtukufu,
Kelele za furaha yuaja Mhashamu mpya Askofu. 
VIII
Kwanini basi ulimi wangu hauachi kuimba,
Jitihada za Bwana wangu zaruhusu kila moyo kuimba,
Hapana, ila kwa kushirikisha upendo na furaha juu ya ono la Muumba,
Mnamo mbili sifuri moja nne mwaka wa Muumba,
Atangazwa kwenda kuanza misioni jimboni Mpanda,
Kuunganisha mioyo pamoja kwa Muumba,
Kutia moyo wote waamini vikwazo kuvishinda,
Vile ambavyo vyaweka mbali ufalme wa Muumba,
Hasa pale maisha yanapodai wa damu ushuda. 
IX
Kama manyoya ya Tai mikono hewani hujongesha,
Bila ya jaribu wala kwa tamaa kukatisha,
Mnamo ishirini na moja Disemba, baraka na furaha kukaribisha!
Mnamo ishirini kumi na nane kwa hamasa mapendo yalinyesha,
Kisha si watoto si wazee walicheza bila kujali kiti, wakifurahisha!
Filimbi, ngoma na mdundo vilivuma juu chini vikidumisha,
Vyote vikifunua mioyo inayofurahisha,
Kupitia mikono iliyokuja na ustadi bashasha. 
X
Oo tazama makunyanzi yakiharibu nyuso za tabasamu,
Kadiri utume ulivyobariki mapito ya ajabu,
Yakisindikizwa bila ya majidai bali nguvu za Mungu ajabu,
Ikifunguka mikono ya kibaba iliyo wazi, pana na ya adabu,
Mkono utoao baraka wala si karaha kwa wajibu,
Mikono ya kibaba isemayo watoto karibu,
Ikiipa miguu ujasiri wa kuanza utume wa kuhudumu,
Kwa busara na kupitia ruhusa halali na adhimu. 
XI
Kisha tazama pande zote ikasikika sauti ikiita,
Neema si bidhaa za kupigia mnada hata,
Mapema kutangaza jina ni Jimbo kupata,
Kufumba na kufumbua neema ya Jimbo Kuu tukapata,
Jina Jimbo kuu matunda yake Mungu neema,
Iliyoambatana na upendo na furaha ya baba mwema,
Kuinjilisha wenye hali ngumu ya maisha, utume si lelemama,
Bila kujali kikwazo au changamoto hakika atenda hima,
Kwa uwepo wa upendo wa Mungu, mara kwake kulinda daima. 
XII
Taratibu zinaita ngoma, ndani na nje kwa ajili ya nani?
Si mwingine ni Mwandamizi mkuu wa Skauti jamani,
Aliipa Skauti weledi usiokoma na matumaini,
Na kuisimamisha kama tanuru iwakayo kwa Imani,
Akiipa maana, matamanio na kazi za vijana maishani,
Kuwapa hamasa vijana na wazee kwa umakini,
Ambamo nidhamu na maadili hushuhudiwa akilini,
Kufikia mafanikio azizi na kutupa mwelekeo maishani.
XIII
Japo kitambo kidogo enyi masikio sikiliza,
Subiri si kwa chuki ujumbe una nini sikiliza,
Wimbo unasogea karibu na Motto wa Jimbo Kuu kukujuza,
Ujumbe wenye nguvu, azizi huwezi pata dukani uliza,
Msingi wake umejengwa katika Neno linalotakatifuza,
Kwa nguvu za kimbingu umejishikiliza,
Kwa ukweli katika kazi aliyopewa na Mungu ukijieleza,
Hakika ndiyo utume, kwa utendaji wa juu akitimiza.
XIV
Upendo wa Kristo unatusukuma,
Ukinong’oneza Kauli mbiu kwa wema,
Nzuri kabisa kama Grotto ya Maria Mama,
Isiyona waa kama asubuhi ya nyota njema,
Umejaliwa baba vipaji vya ajabu na mema,
Vishangazavyo dunia daima,
U mwonekano wa kiongozi mwema,
Ukipokea msururu wa watoto katika lango la wema,
Kwa tabasamu la upendo na furaha ya daima,
Ili wote washiriki chakula pamoja nawe daima,
 Waje kuonja furaha ya sahani moja ya wako wema. 
XV
Hapa yupo mwenye mawazo chanya na mwalimu wa heri,
Mpole, mtumishi, na mhubiri mashuhuri,
Akisimama kikakamavu kupambana na wenye shari,
Shari iwezayo haribu kazi takatifu za watu shwari,
Au kuleta uadui katika umoja wa Kanisa mahiri,
Au uovu unaopambana kudhuru maadili ya wanachama kwa shari,
Hasa dunia itikisikapo kwa macho ya tafiri,
Ikitafuta kutenga watu na kuwapa uchungu kwa shari, 
XVI
Kuwa makini uone tabia ya kushangaza ya kiongozi,
Ambaye kila siku husimama imara kama tulivu ngazi,
Kwa moyo unaoalika na akili ya mtazamo chaya na wazi,
Kusaidiwa na moyo wa msamaha kama upepo azizi,
Usioruhusu mipaka yoyote ya kibaguzi,
Moyo uwapao wote umoja kwa neema na ujuzi,
Kuwabakiza kwenye neema na kufunua maisha ya uwazi.
XVII
Kumbuka walau mara moja puliza filimbi ya kiafrika,
Ikifunua yako heshima, diplomasia na kwako kuaminika,
Bila uwazi wako mashauri yako chanya kusahaulika,
Lakini siyo kwa vilema bali kwa fadhili umesifika,
Ewe mpendwa Askofu wetu Mkuu baba mtukuka,
Miongoni mwa mengi uliyotenda, machache akili yakumbuka,
Kuyafahamu hayo makubwa, ambayo kwayo yamefanyika,
Na neema ya Mungu uliyopokea kiaminifu uwe nayo ushirika.
XVIII
Kifua mbele, Mama Kanisa abaki nawe,
Hakuna gharama yoyote, ya pongezi kwako wewe,
Picha pekee ya mtu ambaye hakuwahi pima wala hesabu wewe,
Kwa kuthaminiwa upendo pekee umetolewa kwako wewe,
Endeleza shirikisha baraka ulizojaliwa wewe,
Na mwendelezo huu usichukuliwe na askari yeyote kamwe,
Yamkini nguvu na nyimbo za vitisho viwe,
Kubwa kiasi gani usiwe na hofu nawe,
Ambaye tayari kasahau kuwa awe,
Hakuna awezaye choma hema ya Munguwe. 
XIX
Ndani na nje ya nchi baba jina lako lasafiri,
Laandikwa kwa mkazo ukutani na kwa ustadi mahiri,
Na liwe kama Mkufunzi wa Skauti, Askofu au Padiri,
Au liwe la Raisi wa TEC au Askofu Mkuu jasiri,
Ila kubwa kuliko yote upatikanapo uaminifu wa mtu mahiri,
Kwa Mungu, watu, na kazi iletayo hazina iliyo nzuri,
Kwa ajili hiyo zasikika sauti za furaha na nzuri,
Aa! Kwa moyo mmoja, jina lako na maisha yako tutayaiga vizuri.
XX
Kwa sauti, midomo ya shukrani yaja kwako ee Mungu,
Kwa upendo wako ambao daima unatoa neema ya kimungu,
Kisha watoto waomba baraka kwa ajili ya baba yao ndugu,
Ambaye mikono yake ya kibaba huunganisha mataifa kidugu,
Hekima yake huvunja katika kila lango usingizi na tepe la wingu,
Hali akiwakaribisha wote maskini na tajiri lango la Mbingu,
Kisha bariki na angaza utume wa baba yangu,
Na vyote vifanyike kwa matakwa yako Mungu,
Na ulivyoviweka katika bakuli lako wewe Mwenyezi Mungu. 
XXI
Sasa! Sikiliza sauti ya kipenga yaja taratibu kuweka koma,
Kwa juhudi kubwa twamkabidhi Baba yetu kwa Bikira Mama
Na pia, kifuani kwa Mbarikiwa sana Mama,
Ili daima mtoto wako awe mwema Ee Mama,
Na kwa moyo mkunjufu tunasali kwa sauti tukisema,
Ee Malkia Mzuri Sana, simamia njia ya Baba Yetu daima,
Na kamwe Usimruhusu aende tofauti nawe Mama,
Abaki katika ulinzi wako daima,
Kwa maana hakuna pa utulivu daima
Zaidi ya kubaki katika usimamizi wako, Ee Mama Mwema,
Na kwa moyo mmoja tunaomba hima,
Umfunike kwa pendo lako pekee Mama,
Kwa kuwa jina lako ulimwenguni Mama,



https://joenwaogbu1.blogspot.com/2020/02/usilie-basi-by-joseph-c-ogbu-joenwaogbu.html


https://joenwaogbu1.blogspot.com/2020/01/chaguo-langu-pendo-langu-na-joseph-c.html

No comments:

Post a Comment

SMILE ON THE FACE; BUT...? by Fr. Joseph C. Ogbu

Imagine! Calmly water turning thicker than blood, Evils gently overflowing like flood. God! be merciful on your precious world, And allow n...