Ujio wa
Askofu Mkuu ni wasifu mfupi wa Askofu Mkuu Gervas John Mwasikwabhila Nyaisonga
wa Jimbo Kuu Katoliki la Mbeya-Tanzania.
Ni kitabu kilichoandikwa kwa mistari
na vina (kisarambe) ikionesha wasifu wa Askofu Mkuu.
*********
Nawashukuru Mafrateri Victor Basilius na Charles
Mtuka walioshirikiana nami katika kutafisiri kitabu hiki kwa Kiswahili.
I
Kwa midomo ya shukrani kwako Mungu twafika,
Kwa upendo wako kichwa chaneemeka,
Mwili wako dhidi ya ugonjwa na kifo akufunika,
Siku zaja pamoja na paji ili
kukua na kuzeeka,
Usiku na mchana vyakufanya mwenye
fadhili hakika,
Kutangazia uimara mioyo
iliyopondeka,
Kupitia moyo uliowekwa mamlaka,
Ustadi wa Mungu umeoteshwa na
kudhihirika.
II
Hapa ni wimbo uelezao ukuu na
ukweli wa Mtumishi,
Afanyaye kazi kwa umakini asiye
mshabiki bali Mtumishi,
Alizaliwa Novemba, mwezi
mbarikiwa wa kuishi,
Tarehe tatu, mwaka moja tisa sita
sita, wa mema matashi,
Kuvutia dunia siku ya kwanza kwa
kilio pako pa kuishi,
Si tu furaha kwa familia hata
wapita njia hawakanushi,
Mbozi-Mbeya kulisikika bila wa
binadamu ushawishi,
Yote chini ya ulinzi wa Mungu
Tarishi.
III
Safari ya maisha kuwa ya kimungu
ilijidhihirisha,
Ni katika mwaka huu
tunajikumbusha,
Moja tisa nane mbili na moja tisa
nane tisa kisha,
Elimu ya msingi na sekondari kakamilisha,
Kafanya mpango wa kimungu,
tulivu, ajabu wa kutafakarisha,
Seminari kuu kuwasili kuwa na
moyo na wito haikutosha,
Ni upendo wa Mungu na ufadhili wa
Askofu ulimwezesha,
Waliongoza hatua zake mpango
kukamilisha,
Ili maisha yasiachane na utakatifu
wake wa maisha.
IV
Ndoto zadhirisha ukweli, na sauti
za pekee zasikika,
Na midomo vyaimba kwa sauti isiyo
linganishika,
Kumkaribisha katika Altare
takatifu mtu aliyetukuka,
Bila ya gharama yoyote paji lake
ni chapa isiyofutika,
Kurejea tukio la moja tisa tisa
sita lile lililosifika,
Ilikuwa Julai kumi na moja tarehe
iliyotukuka,
Ni siku ile ya upadirisho kwa
Imani alisifika,
Akiwa na nguvu thabiti kutangaza
neno na Imani iliyoimarika,
Ikikuza ukweli wa mbingu nakukata
kama upanga wa shujaa hakika.
V
Hakika, amesimama siku zote
katika utume,
Kihalali alifikia upadre kuonesha
wake utume,
Kutoa neema za kibaba kama wakili
paroko kiutume,
Atoa furaha na Sakramenti kwa
kanisa la kitume,
Huduma yake ya upendo
yadhihirisha uzuri wa utume,
Afanya kazi kwa neema na shime,
Kwake ujasiri, haki na amani
sehemu ya utume,
Kuwapigania waliokataliwa na
kuwapa shime.
VI
Utume umeimarika kwa neema
itokayo juu kwa baba,
Si tu kuwa mlezi Seminari bali
kuwa Mwalimu na baba,
Na kufanywa Mkufunzi na kuwa
kichwa haya si haba,
Mwenye ufahamu na kuwapa ufahamu
kama baba,
Kuwafanya wote mwanga wa kweli
kubeba.
VII
Aha! Kwa upadre wake waweza kuona
ukamilifu,
Wa kibaba ukifunua majukumu yake tukufu
Kisha sikia zumari, filimbi kwa
furaha kamilifu,
Bila kuchoka vikiimba, vikicheza na
kusifu,
Kwa baraka ya tisa machi kwa
Mungu toa utukufu,
Mnamo mbili sifuri moja moja
katika Kanisa Katoliki Takatifu,
Huko Dodoma kusimamishwa
Mchungaji mtukufu,
Kelele za furaha yuaja Mhashamu
mpya Askofu.
VIII
Kwanini basi ulimi wangu hauachi
kuimba,
Jitihada za Bwana wangu zaruhusu
kila moyo kuimba,
Hapana, ila kwa kushirikisha
upendo na furaha juu ya ono la Muumba,
Mnamo mbili sifuri moja nne mwaka
wa Muumba,
Atangazwa kwenda kuanza misioni
jimboni Mpanda,
Kuunganisha mioyo pamoja kwa
Muumba,
Kutia moyo wote waamini vikwazo
kuvishinda,
Vile ambavyo vyaweka mbali ufalme
wa Muumba,
Hasa pale maisha yanapodai wa
damu ushuda.
IX
Kama manyoya ya Tai mikono hewani
hujongesha,
Bila ya jaribu wala kwa tamaa
kukatisha,
Mnamo ishirini na moja Disemba, baraka
na furaha kukaribisha!
Mnamo ishirini kumi na nane kwa
hamasa mapendo yalinyesha,
Kisha si watoto si wazee
walicheza bila kujali kiti, wakifurahisha!
Filimbi, ngoma na mdundo vilivuma
juu chini vikidumisha,
Vyote vikifunua mioyo
inayofurahisha,
Kupitia mikono iliyokuja na
ustadi bashasha.
X
Oo tazama makunyanzi yakiharibu
nyuso za tabasamu,
Kadiri utume ulivyobariki mapito
ya ajabu,
Yakisindikizwa bila ya majidai
bali nguvu za Mungu ajabu,
Ikifunguka mikono ya kibaba iliyo
wazi, pana na ya adabu,
Mkono utoao baraka wala si karaha
kwa wajibu,
Mikono ya kibaba isemayo watoto
karibu,
Ikiipa miguu ujasiri wa kuanza
utume wa kuhudumu,
Kwa busara na kupitia ruhusa
halali na adhimu.
XI
Kisha tazama pande zote ikasikika
sauti ikiita,
Neema si bidhaa za kupigia mnada
hata,
Mapema kutangaza jina ni Jimbo
kupata,
Kufumba na kufumbua neema ya
Jimbo Kuu tukapata,
Jina Jimbo kuu matunda yake Mungu
neema,
Iliyoambatana na upendo na furaha
ya baba mwema,
Kuinjilisha wenye hali ngumu ya
maisha, utume si lelemama,
Bila kujali kikwazo au changamoto
hakika atenda hima,
Kwa uwepo wa upendo wa Mungu,
mara kwake kulinda daima.
XII
Taratibu zinaita ngoma, ndani na
nje kwa ajili ya nani?
Si mwingine ni Mwandamizi mkuu wa
Skauti jamani,
Aliipa Skauti weledi usiokoma na
matumaini,
Na kuisimamisha kama tanuru
iwakayo kwa Imani,
Akiipa maana, matamanio na kazi
za vijana maishani,
Kuwapa hamasa vijana na wazee kwa
umakini,
Ambamo nidhamu na maadili
hushuhudiwa akilini,
Kufikia mafanikio azizi na kutupa
mwelekeo maishani.
XIII
Japo kitambo kidogo enyi masikio
sikiliza,
Subiri si kwa chuki ujumbe una
nini sikiliza,
Wimbo unasogea karibu na Motto wa
Jimbo Kuu kukujuza,
Ujumbe wenye nguvu, azizi huwezi
pata dukani uliza,
Msingi wake umejengwa katika Neno
linalotakatifuza,
Kwa nguvu za kimbingu
umejishikiliza,
Kwa ukweli katika kazi aliyopewa
na Mungu ukijieleza,
Hakika ndiyo utume, kwa utendaji
wa juu akitimiza.
XIV
Upendo wa Kristo unatusukuma,
Ukinong’oneza Kauli mbiu kwa
wema,
Nzuri kabisa kama Grotto ya Maria
Mama,
Isiyona waa kama asubuhi ya nyota
njema,
Umejaliwa baba vipaji vya ajabu
na mema,
Vishangazavyo dunia daima,
U mwonekano wa kiongozi mwema,
Ukipokea msururu wa watoto katika
lango la wema,
Kwa tabasamu la upendo na furaha
ya daima,
Ili wote washiriki chakula pamoja
nawe daima,
Waje kuonja furaha ya sahani moja ya wako
wema.
XV
Hapa yupo mwenye mawazo chanya na
mwalimu wa heri,
Mpole, mtumishi, na mhubiri
mashuhuri,
Akisimama kikakamavu kupambana na
wenye shari,
Shari iwezayo haribu kazi
takatifu za watu shwari,
Au kuleta uadui katika umoja wa
Kanisa mahiri,
Au uovu unaopambana kudhuru
maadili ya wanachama kwa shari,
Hasa dunia itikisikapo kwa macho
ya tafiri,
Ikitafuta kutenga watu na kuwapa
uchungu kwa shari,
XVI
Kuwa makini uone tabia ya
kushangaza ya kiongozi,
Ambaye kila siku husimama imara
kama tulivu ngazi,
Kwa moyo unaoalika na akili ya
mtazamo chaya na wazi,
Kusaidiwa na moyo wa msamaha kama
upepo azizi,
Usioruhusu mipaka yoyote ya
kibaguzi,
Moyo uwapao wote umoja kwa neema
na ujuzi,
Kuwabakiza kwenye neema na
kufunua maisha ya uwazi.
XVII
Kumbuka walau mara moja puliza
filimbi ya kiafrika,
Ikifunua yako heshima, diplomasia
na kwako kuaminika,
Bila uwazi wako mashauri yako
chanya kusahaulika,
Lakini siyo kwa vilema bali kwa
fadhili umesifika,
Ewe mpendwa Askofu wetu Mkuu baba
mtukuka,
Miongoni mwa mengi uliyotenda,
machache akili yakumbuka,
Kuyafahamu hayo makubwa, ambayo
kwayo yamefanyika,
Na neema ya Mungu uliyopokea
kiaminifu uwe nayo ushirika.
XVIII
Kifua mbele, Mama Kanisa abaki
nawe,
Hakuna gharama yoyote, ya pongezi
kwako wewe,
Picha pekee ya mtu ambaye
hakuwahi pima wala hesabu wewe,
Kwa kuthaminiwa upendo pekee
umetolewa kwako wewe,
Endeleza shirikisha baraka
ulizojaliwa wewe,
Na mwendelezo huu usichukuliwe na
askari yeyote kamwe,
Yamkini nguvu na nyimbo za
vitisho viwe,
Kubwa kiasi gani usiwe na hofu
nawe,
Ambaye tayari kasahau kuwa awe,
Hakuna awezaye choma hema ya
Munguwe.
XIX
Ndani na nje ya nchi baba jina
lako lasafiri,
Laandikwa kwa mkazo ukutani na
kwa ustadi mahiri,
Na liwe kama Mkufunzi wa Skauti,
Askofu au Padiri,
Au liwe la Raisi wa TEC au Askofu
Mkuu jasiri,
Ila kubwa kuliko yote upatikanapo
uaminifu wa mtu mahiri,
Kwa Mungu, watu, na kazi iletayo
hazina iliyo nzuri,
Kwa ajili hiyo zasikika sauti za
furaha na nzuri,
Aa! Kwa moyo mmoja, jina lako na
maisha yako tutayaiga vizuri.
XX
Kwa sauti, midomo ya shukrani
yaja kwako ee Mungu,
Kwa upendo wako ambao daima
unatoa neema ya kimungu,
Kisha watoto waomba baraka kwa
ajili ya baba yao ndugu,
Ambaye mikono yake ya kibaba
huunganisha mataifa kidugu,
Hekima yake huvunja katika kila
lango usingizi na tepe la wingu,
Hali akiwakaribisha wote maskini
na tajiri lango la Mbingu,
Kisha bariki na angaza utume wa
baba yangu,
Na vyote vifanyike kwa matakwa
yako Mungu,
Na ulivyoviweka katika bakuli
lako wewe Mwenyezi Mungu.
XXI
Sasa! Sikiliza sauti ya kipenga
yaja taratibu kuweka koma,
Kwa juhudi kubwa twamkabidhi Baba
yetu kwa Bikira Mama
Na pia, kifuani kwa Mbarikiwa
sana Mama,
Ili daima mtoto wako awe mwema Ee
Mama,
Na kwa moyo mkunjufu tunasali kwa
sauti tukisema,
Ee Malkia Mzuri Sana, simamia
njia ya Baba Yetu daima,
Na kamwe Usimruhusu aende tofauti
nawe Mama,
Abaki katika ulinzi wako daima,
Kwa maana hakuna pa utulivu daima
Zaidi ya kubaki katika usimamizi
wako, Ee Mama Mwema,
Na kwa moyo mmoja tunaomba hima,
Umfunike kwa pendo lako pekee
Mama,
Kwa kuwa jina lako ulimwenguni
Mama,
Daima utabaki kubarikiwa na kupewa heshima.