Yangu
ni kukushukuru; Na wala si kukufuru,
Magoti
chini nakuomba; Baba tusafiri sambamba,
Mkono
wako wa nguvu; hakika huponya maumivu,
Naomba
niseme asante; bila Wewe dunia haifai
lolote,
Asante
Baba kwa maisha; mengi bora menihifadhia kwa bahasha,
Nyumba
hata sina kabisa; na sielewi wapi nipate tena hisa,
Lakini
utajiri hushuka kama umande; kwa kuwa Baba haangalii upande,
Loo!
Kumbe mimi ni tajiri sana; basi kamwe Baba sitakutukana,
Siku
zote furaha moyoni; amani rohoni na afya mwilini,
Haya yote kabisa si haba; nasema asante ee Wangu Baba,
Kwa
kuwa umenifanya mtajiri; hata kama pesa imegoma
kuja alfajiri,
Asante
sana Baba Yangu; kwa zawadi yako mlangoni mwangu,
Basi
tusimame wote wadau; tuchezecheze bila kusahau;
Kujitunza
katika upendo na amani; ndo utajiri wa
kwanza maishani,
Daima
mikono itaelekea juu; kukushukuru Wewe
uliye na Ukuu,
Kwa
kufanya ulimi kuonja huu utajiri; kwa kuwa huo ndio safi ujasiri,
Lakini daima sitamsahau Mama Mpenzi; Bikira Maria, Mama Safi Sana,
Mwombezi wangu; mahitaji yangu, yote kayafikisha kwa Mungu,
Asante Sana Mama, Mimi na Wewe daima.
