Peke
yako, sitakuacha
Wewe
upendo, sitakuficha.
Upendo
hujenga maisha yawe imara,
Kabisa
kupenda haina hasara.
Nashangaa
tena hauna hata tabaka,
Ila
ndani hujazwa tupu baraka.
Loo!
zawadi kubwa sana tulizojaliwa,
Kugawia
wenye nguvu na waliolemewa;
Sawa
kwa wakubwa na pia kwa wadogo.
Tukijua
upendo una nguvu si kidogo;
Basi
Upendo mikononi tushike sote,
Ili
dunia iendelee kumeremeta kwa wote.

Kudos! Kudos!! Kudos!!!
ReplyDeletekaka yangu
Amina sana bro. Na hakika ushakuwa mswahil
ReplyDeleteHakika "upendo mikononi tushike sote, ili dunia iendelee kumeremeta kwa wote"
ReplyDeleteKida Sir., Hongera sana
Amina,Mungu azidi kutubariki
ReplyDeleteAmina,Mungu azidi kutubariki
ReplyDeleteHakika kukiwa na Upendo bc dunia nzima itameremeta! Barikiwa sn
ReplyDelete