Tanzania wewe ni nuru, Sote tusherekee Siku ya Uhuru,
Furaha twatakie tele, Baraka nyuma na mbele,
Milele Mtasimama imara, Umoja mfurahie kila mara,
Furahieni nyote wazalendo, Nchi inaongozwa kwa upendo,
Ee Mungu wetu Mkuu, Wabariki na uwaweke Watoto wako juu,
Wawe kama taa juu ya mnara, Na Maisha mazuri bila hasara,
Basi, Baba Ubariki Tanzania, Waendelee kuipenda Nchi na kuifarahia,
Twatakieni Sikukuu njema, Na yote mazuri mema,
Uishi daima Tanzania, Mbarikiwe Sana Watanzania.

Asante mkuu ubarikiwe
ReplyDeleteAsante sana Bro.
ReplyDeleteπππππ
ReplyDelete