Bora uchukiwe sababu ya wivu
Utokanao na wako mfano bora
Si kwa sababu kutokujitahidi na uvivu
Au kuchukia kazi na kulala kila mara.
Simama, vaa mkanda; acha kushika mashavu
Usiogope, kila siku inatujia na yake nguvu
Maisha mazuri sana, kabisa si mabovu
Kazi hazikwepeki; mweke Mungu mbele, bila ulegevu.
Hekima ya Baba iendelee kudumu milele
Inasikika masikioni bila hata kelele
Na hu i pa miguu nguvu kusonga mbele
Na daima huua maovu kama mshale.
…...…..................................................................
....................................................
Wazo lililotengenezwa kutoka kwa maneno ya Baba Askofu Mkuu Geravas M. Nyaisonga,
28/09/2021

Hakika idumu na kudumu,
ReplyDeleteIsipite bila ya umuhimu,
Wa leo umuhimu kesho hukumu,
Dhamiri kipimo cha ukweli mgumu!
Wooow! Shukrani Sana, fundisho katupatia tena.
DeleteUtunzi bora timamu,kongole kwako baba,
ReplyDeleteKiswahili mehitimu, wakijulia si haba,
Ukawe mwema mwalimu,katapike uloshiba,
Hongera ogbu hongera, kipaji chako ni lulu.
Bila kuwa na haraka, naomba niseme asante Kaka, na Mungu Mwenyezi awakinge na awajalie baraka.
DeleteOlomi wangu mkono, twende tukampongeze,
ReplyDeleteUtari uso kikomo, karama aendeleze,
Havitukifu vigano, vya Radha bila ya zeze,
Ogbu zako kongore, zidi kutupa nasaha
Hahaha, mwalimuu tayari kaandika, wanafunzi sasa tutulie; hakuna namna, kuelewa ngumu, basi tusilie; misamiati migumu,anakuja kutuelezea, hahaha tuvumilie. Shukrani Sana Baba kwa comment yako!!! Pamoja Sana Baba.
Delete