Habari njema imetufikia; Watanzania furahini
Mapadre,watawa, walei, sote simameni
Tutazame tulikotokea, tulipo na tunapoelekea
Kweli, furaha kubwa kwetu Tanzania.
Sinodi ya Maaskofu; Mkutano Mkuu wa Mababa
Kaitisha yule Mkuu, Francis wetu Papa
Imani yetu idumu, mpaka tufike kwa Baba
Liishi Kanisa letu, lisafiri bila kusimama.
Kumbe ndo kinachoendelea katika Kanisa
Nasi tuko imara kushiriki kabisa
Tutembee pamoja sote katika umoja
Tusiache fuatilia, kila hatua-na-hoja.
Kwa pamoja na ushirikiano tutaweza
Katika umoja tutafurahi na kucheza
Sinodi hii, ya ulimwengu wote
Njooni haraka tutembee pamoja sote.
Mashaka ondoeni, wasiwasi fukuza
Pamoja tusafiri, sikubali kuachwa
Nyuma we sibaki, tukalijenge Kanisa
Umoja Sinodi, uwazi, ukweli kila hatua.
Kina baba na mama, furahini
Amka wewe kijana, watoto msibaki
Amkeni mliolala, mbiu yapigwa Sinodi
Si ndoto tena, sinodi i mlangoni.
Wako mchango muhimu, msaadao hakika
Uthamini ee ndugu, dumisha ushirika
Kwa nini usishiriki? Sipishane na baraka
Tumikia Kanisa hili, na thawabu tapata
Majimbo yote, njooni mchote baraka
Msisite, msichelewe kabisa; kimbieni haraka
Mama Kanisa anayofuraha kusema; karibuni
Na msiogope Kupiga hodi nyumbani.
Wapendwa, tusikilizeni utaratibu wa majimbo yetu
Tuweze kulisaidia Kanisa kwa utaalamu wetu
Kwa unyenyekevu na upendo wa dhati
Ili tuendelee kufurahia ulimwengu kama Umati.
(Sinodi ya XVI ya Maaskofu kiulimwengu 2021-2023)
ππ
ReplyDeleteππ
DeleteπAmina Kuuπ
ReplyDeleteππ
DeleteShukrani babaa mwema
ReplyDeleteMungu Mwenyezi ndo Mwema Babaππ.
Deleteππππππ
Asante sana
ReplyDeleteπππ
DeleteBaba Ogbu, kongere tutajitahidi kushiriki hasa kwa sala
ReplyDeleteπ☺️π
Delete