Tuesday, 4 August 2020

NAKED DANCER by ValTony Ogbu

Naked dancers on the street
Strippers even in the house of the maker.
And you call this modernity and fashion?
Indeed the whole saga begs clarity.
You walk half clothed; exposing contours 
At the mercies of the devouring vultures
Mocking the very subtleness of your nature.

Your words lure flies from all corners 
Your vulgarism naughtily your boldness.
Oh! How little would your feeble mind know
How these revered words carelessly thrown
Name you, a victim of inordinate pleasure.

Your steps mock the dignity of our ancestry 
Prodigies of ugly trend; 
Exposing the rivulets of your virginities
Selling your wares to unworthy buyers 
In cornered street without mutual bargains. 

Your major customers become "gluttony"
Men with unsuited personality and loose principles.
And you cry, ASSAULT!
When your accursed fashion directs their act.

Yes! The crime is a crime, no excuse 
But the streets are flooded with thousand of naked souls 
And uncensored minds
Urging them on and on
For an improper but " palatable" meal on the table of abuse.

Monday, 6 July 2020

JoenwaOgbu

BADO IPO, HAIJAPOTEA na Joseph C. Ogbu (JoenwaOgbu)

Naomba toa mkono kidevuni
Na ufute machozi mashavuni,
Nini haki yako unawaza imepotea
Muamini Mungu tu atakurudishia,
Maisha haya ndo kawaida yake
Ni kama fumbo maanayake,
Acha kufadhaika, ni muda wa kutabasamu
Furahi! Mungu hatakuacha kwenye jamu,
Basi simama, Mama anakuita! Toka kwenye mahangaiko yako
Na ujue daima, Mama na Mwanaye hawataacha kuwa Wasaidizi wako.

Friday, 3 July 2020

ETI,VIJANA LEO SIYO YENU NGOJENI KESHO! na John K. Semindu



Eti,vijana leo siyo yenu ngojeni kesho! Hahahaha... Msemo huu hauna tofauti na ule usemao “Vijana ni taifa la kesho”! Mnanitia uvivu kutumia nguvu, akili na vipaji vyangu kufanikisha mambo kwa kuingojea kesho yenu isiyofika. Hivi kesho ilishawahikufika? Na ikishafika Inaitwaje? Ikikaribia haiitwi tena kesho hiyo ni leo, ndiyo sasa. Na siku ile uliyoitumia kusema kesho itaitwa jana. Kesho iko wapi? …haaaaaa!.. ndiyo ile imeitwa jana au ndiyo hii inaitwa leo? Wewe kesho, mbona hufiki? Kumbe jana ni halisi na leo pia ni halisi kwamaana jana imepita na leo ndiyo sasa, lakini kesho haijafika. Hakika kesho haijawahi fika, kesho haijawahi kuwa, inabaki akilini tu. Kesho uniache, mimi najituma sasa.

Utasikia mmoja anasema, ndugu yangu nivumilie kidogo kesho nitakupatia mzigo wako; na mwingine anasema, rafiki kesho nitakutumia pesa kidogo. Hizi ni baadhi ya kauli za kuleta matumaini kuifikia kesho japo haifikiki. Atakapokupatia mzigo wako siyo tena kesho bali ni leo;  akikutumia pesa siyo tena kesho bali ni sasa. Kesho itaendelea kubaki kwenye akili na siyo kwenye uhalisia.                                    Nifupishe tu maneno, kwamba kesho haifiki daima. Hata uwe na mbio kiasi gani huwezi kuifikia kesho, na hata uwe mrefu wa futi nane kama Robert Wadlow huwezi kuiona kesho. Labda wanasayansi watusaidie ndege za mwendokasi tuikimbize; wenzenu wa Dar-essalaam wana mabasi ya mwendo kasi lakini mpaka sasa bado hawajaifikia kesho. Labda Flyovers zitawapa matumaini ya kuifikia kesho.

Falsafa hii ya maisha (vijana taifa la kesho) inanyima fursa na kudogosha vijana katika bidii za kuleta maendeleo katika jamii. Kauli hii hufubaisha fikra kwa vijana na kupelekea vijana kungojea kupewa amri na kufanyiwa vitu vingi bila wao kushiriki kikamilifu au kujituma kikamilifu kwa maana leo siyo yao wanangoja kesho ambayo haijawahi kufika.

Kauli hii inatoa fursa zaidi kwa wale walio vuka umri wa ujana (watu wazima) kuwadharauna kuwadogosha vijana katika kutoa mawazo, mapendekezo na hata kusimamia misimamo yao katika maisha ya kila siku. Nazani ulishawahi kusikia au kuambiwa “utatuambia nini? Wewe bado kijana sana, subiri ukue ndiyo utoe mawazo, tusikilize sisi wazee kwanza”. Sitaki kukwambia usiwasikilize wazee bali ninyi mlio wazee wapeni vijana nafasi ya kutoa mawazo bila kuwabeza kwa kauli za namna hiyo maana vijana wana fikra motomoto. Ndiyo kusema kwamba, malumbano mengi na misuguano hasi ya kimawazo kati ya vijana na watu wazima huanzia kwenye falsafa hii ya vijana taifa la kesho au kusema vijana leo siyo yenu ngojeni kesho.

Mimi niliye kijana ninayesukumwa na moyo wangu kuhitaji usalama, uhuru, kufaulu, utulivu moyoni na kupata heshima ndiye taifa la sasa, leo ndiyo yangu kwa maana natambua kwamba kesho haijawahi kufika na hata ikifika siyo tena kesho na ikipita siyo tena kesho. Vijana muda ni sasa tusingoje kesho...! Tusipumbazwe na kauli "vijana taifa la kesho" hii itafaa kwa watoto. Nasema tena, achana na falsafa ya ngoja kesho wewe ni taifa la sasa.
Vijana leo ndiyo yetu, kesho haifiki.

SMILE ON THE FACE; BUT...? by Fr. Joseph C. Ogbu

Imagine! Calmly water turning thicker than blood, Evils gently overflowing like flood. God! be merciful on your precious world, And allow n...