Friday, 28 January 2022

MACHOZI NA MAJONZI TENA na Shemasi Joseph C. Ogbu (JoeNwaOgbu)

 Nyumbani imesikika, 
Mlango ukapigika,
Kelele kubwa metoka,
Mjumbe ameshafika,
Machozi yatiririka,
Moyo umeshavunjika,
Loo! Baba Mwanjonde katoka.

Baba Mwanjonde katoka,
Kenda kwa alompeleka,
Alofanya kaumbika, 
Ni huzuni kwa hakika,
Kwake Mungu atapumzika,
 Imani yetu kafika,
Kweli hatuna mashaka,
Bwana ndiye kamtaka.

Bwana ndiye kamtaka,
Alotufanya kucheka,
Kwa upole alipendeka,
Utume alisifika,
Baridi imekushika,
Joto kwako limetoka,
Mtu mwema kaondoka,
Mwanjonde ametutoka.

Mwanjonde ametutoka,
Ulimi umekauka,
Kwa tenzi tunatenzika,
Huzuni na hekaheka,
Ni wazi na ni hakika,
Nasi huko tutafika,
Padre Timothy nenda,
Nenda salama Mwanjonde.

Hatuna cha kulaumu, 
Mungu kwake ziwe sifa,
Sote tulo binadamu,
Ni hakika tutakufa,
Hakuna sintofahamu,
Mwanjonde metangulia,
Na kesho tutamfuata.

Kwaheri Baba
Kwaheri Sana Baba
Safari umemaliza Baba
Lala salama Baba
Nasi baadayi tutakufuata Baba.

17 comments:

  1. Hongera sana kaak Joseph, ujumbe mzuri sana. Padre Mwanjonde apumzike kwa amani.

    ReplyDelete
  2. Ujumbe mzr sana brother joseph, pumzika kwa amani father mwanjonde

    ReplyDelete
  3. Pumzika kwa amani baba Timothy Mwanjonde

    ReplyDelete
  4. Mweshimiwa sana baba Shemasi tunakushukuru kwa ujumbe mzuri sana hakika Padre Mwanjonde amelala mahari pema peponi....Fr Timothy apumzike kwa amani

    ReplyDelete
  5. Hongera Sana Baba Shemasi kwa ujumbe nzuri. Baba yetu mpendwa Apumzike kwa Amani katika Kristo.

    ReplyDelete
  6. Hongera sana kwa utenzi mzuri, na poleni kwa kumpoteza mmoja wenu. Roho ya marehemu ipumzike pema peponi
    Amina

    ReplyDelete
  7. Kwa kweli ni pigo kubwa. Tumwombee apumzike katika Amani ya Bwana.

    ReplyDelete
  8. Slots Provider Review ᐈ Best Casino Bonus Codes 2021
    Slots Casino 다이사이 Bonuses for Desktop and Mobile · 1. Bovada: 250% Welcome Bonus up to £400 해축 보는 곳 · 윌리엄힐 2. Caesars Casino: 50% Welcome Bonus up to €1,600 · 3. Bet365: 50% Welcome Bonus up bwin to 리턴 벳

    ReplyDelete

SMILE ON THE FACE; BUT...? by Fr. Joseph C. Ogbu

Imagine! Calmly water turning thicker than blood, Evils gently overflowing like flood. God! be merciful on your precious world, And allow n...