Nyumbani imesikika,
Mlango ukapigika,
Kelele kubwa metoka,
Mjumbe ameshafika,
Machozi yatiririka,
Moyo umeshavunjika,
Loo! Baba Mwanjonde katoka.
Baba Mwanjonde katoka,
Kenda kwa alompeleka,
Alofanya kaumbika,
Ni huzuni kwa hakika,
Kwake Mungu atapumzika,
Imani yetu kafika,
Kweli hatuna mashaka,
Bwana ndiye kamtaka.
Bwana ndiye kamtaka,
Alotufanya kucheka,
Kwa upole alipendeka,
Utume alisifika,
Baridi imekushika,
Joto kwako limetoka,
Mtu mwema kaondoka,
Mwanjonde ametutoka.
Mwanjonde ametutoka,
Ulimi umekauka,
Kwa tenzi tunatenzika,
Huzuni na hekaheka,
Ni wazi na ni hakika,
Nasi huko tutafika,
Padre Timothy nenda,
Nenda salama Mwanjonde.
Hatuna cha kulaumu,
Mungu kwake ziwe sifa,
Sote tulo binadamu,
Ni hakika tutakufa,
Hakuna sintofahamu,
Mwanjonde metangulia,
Na kesho tutamfuata.
Kwaheri Baba
Kwaheri Sana Baba
Safari umemaliza Baba
Lala salama Baba
Nasi baadayi tutakufuata Baba.
Hongera sana kaak Joseph, ujumbe mzuri sana. Padre Mwanjonde apumzike kwa amani.
ReplyDeleteAmina. Shukrani Sana Kaka
DeleteUjumbe mzr sana brother joseph, pumzika kwa amani father mwanjonde
ReplyDeleteAmina. Asante sana
DeletePumzika kwa amani baba Timothy Mwanjonde
ReplyDeleteAmina
DeleteMweshimiwa sana baba Shemasi tunakushukuru kwa ujumbe mzuri sana hakika Padre Mwanjonde amelala mahari pema peponi....Fr Timothy apumzike kwa amani
ReplyDeleteAmina. Shukrani sana
DeleteBaba shemasi Asante sana
ReplyDeleteShukrani Sana Ndugu
DeleteHongera Sana Baba Shemasi kwa ujumbe nzuri. Baba yetu mpendwa Apumzike kwa Amani katika Kristo.
ReplyDeleteAmina. Daalu rine Nwanne
DeleteHongera sana kwa utenzi mzuri, na poleni kwa kumpoteza mmoja wenu. Roho ya marehemu ipumzike pema peponi
ReplyDeleteAmina
Amina. Shukrani Sana Kaka
DeleteKwa kweli ni pigo kubwa. Tumwombee apumzike katika Amani ya Bwana.
ReplyDeleteAmina. Asante Sana
DeleteSlots Provider Review ᐈ Best Casino Bonus Codes 2021
ReplyDeleteSlots Casino 다이사이 Bonuses for Desktop and Mobile · 1. Bovada: 250% Welcome Bonus up to £400 해축 보는 곳 · 윌리엄힐 2. Caesars Casino: 50% Welcome Bonus up to €1,600 · 3. Bet365: 50% Welcome Bonus up bwin to 리턴 벳