Huzuni kapata umaarufu haraka,
Tanzia! barua likasomeka,
Macho yalitiwa upofu, kwa machozi kutirika,
Alfajiri sana Jeshi kaondoka
Wala adhuhuri hukuweza fika.
Furaha yetu ilipojituliza
Huzuni ikapaaza sauti,
Tamaa yetu tungekuuguza,
Ila haikutuonea huruma mauti,
Utume kweli ungeendeleza,
Basi Kifo naye msaliti.
Loo! Dunia basi
Machozi yetu kasi
Padre tena haupo nasi
Imani umeilinda
Kristo Mauti lishinda
Na huko kwake mekwenda,
Na Kwake umejituliza.
Hakika kifo ni fumbo
Wala hatuelewe lake jambo.
Padre wetu Asterius Mutegeki
Sauti yako tena haisikiki,
Katamani kabisa tucheke
Wazo la uwepo wake,
Ndo kaja Mwenyezi aliyemtaka
Nasi tukabaki na kuchoka.
Katika wema na kheri,
Mpe taji jemadari,
Kwenye udhaifu na shari,
Huruma yako itakabali,
Twaomba astahili,
Umuangaze kwa yako miali,
Astahili rehema zako.
Lala salama Baba,
Usafiri salama Mtu mwema
Naenda salama Mpendwa
Tutakutana kwa Mungu Baba.

Vizuri sana
ReplyDeleteTumshukuru Mungu kwa Zawadi ya Padri Asterius Mutegeki! Mwendo ameumaliza...! APUMZIKE KWA AMANI.
ReplyDeleteMwenyezi Mungu ameamua. Asante Baba Joseph kwa shairi zuri lakini ni la simanzi.
ReplyDeleteMay his soul rest in peace. Amen. It is a pity indeed.
ReplyDeleteMay rest in peace
ReplyDeleteApumzike kwa Amani. Pole sana Kwa msiba mkubwa
ReplyDeleteTunamshukuru Mungu. Mungu amemchuma ua lake lingali bado changa.
ReplyDeletePumzika kwa Amani padre
ReplyDeleteTunamshukuru Mungu Kwa zawadi ya maisha ya fr Mtegeki imempendeza Mungu kuchuma us changa likamtumikie Mbingun nasasa tumepata mwombez wetu mbingun ๐ nenda baba tutaonana badae
ReplyDeleteHkweli Duniani tu wapitaji.Pumzika kwa Amani Baba.
ReplyDeleteApumzike kwa Aman ni mapema sana ๐ญ๐ญ
ReplyDeleteShairi nzuri lenye kusikitisha na huzuni kubwa pumzika kwa Amani padre
ReplyDeleteAminaaa ๐ญ๐ญ pumzika kwa amani
ReplyDeleteMungu ampe pumnziko la milele!
ReplyDeleteMwenyez MUNGU amjalie pumziko la milele
ReplyDeleteMarehem apate rehema kwa mungu apumzike kwa amani๐๐
ReplyDeleteDah ni mapema mnoo๐ญ๐ญ
ReplyDeleteRIP amen ๐๐๐
DeleteApumzike kwa Amani.
ReplyDeleteKuna wakati wa kupanda na wakati wa kuvumuli
ReplyDeleteR.I.P
ReplyDeleteBlog ipo vizuri sana.tuendelee kuitumia,pia nimeona kipaji chako,kweli haubahatishi
ReplyDeleteRIP mpendwa wetu
ReplyDelete