Monday, 21 August 2023

MAPEMA SANA PADRE na Fr. Joseph C. Ogbu

Huzuni kapata umaarufu haraka,
Tanzia! barua likasomeka,
Macho yalitiwa upofu, kwa machozi kutirika,
Alfajiri sana Jeshi kaondoka 
Wala adhuhuri hukuweza fika.

Furaha yetu ilipojituliza
 Huzuni ikapaaza sauti,
Tamaa yetu tungekuuguza,
Ila haikutuonea huruma mauti,
 Utume kweli ungeendeleza,
Basi Kifo naye msaliti. 

Loo! Dunia basi
Machozi yetu kasi
Padre  tena haupo nasi
Imani umeilinda
Kristo Mauti lishinda
Na huko kwake mekwenda, 
Na Kwake umejituliza.

Hakika kifo ni fumbo
Wala hatuelewe lake jambo.
Padre wetu Asterius Mutegeki
Sauti yako tena haisikiki,
Katamani kabisa tucheke
Wazo la uwepo wake,
Ndo kaja Mwenyezi aliyemtaka
Nasi tukabaki na kuchoka.

Katika wema na kheri,
Mpe taji jemadari,
Kwenye udhaifu na shari,
Huruma yako itakabali,
Twaomba astahili,
Umuangaze kwa yako miali,
Astahili rehema zako.

Lala salama Baba, 
Usafiri salama Mtu mwema
Naenda salama Mpendwa
Tutakutana kwa Mungu Baba. 

23 comments:

  1. Tumshukuru Mungu kwa Zawadi ya Padri Asterius Mutegeki! Mwendo ameumaliza...! APUMZIKE KWA AMANI.

    ReplyDelete
  2. Mwenyezi Mungu ameamua. Asante Baba Joseph kwa shairi zuri lakini ni la simanzi.

    ReplyDelete
  3. May his soul rest in peace. Amen. It is a pity indeed.

    ReplyDelete
  4. May rest in peace

    ReplyDelete
  5. Apumzike kwa Amani. Pole sana Kwa msiba mkubwa

    ReplyDelete
  6. Tunamshukuru Mungu. Mungu amemchuma ua lake lingali bado changa.

    ReplyDelete
  7. Pumzika kwa Amani padre

    ReplyDelete
  8. Tunamshukuru Mungu Kwa zawadi ya maisha ya fr Mtegeki imempendeza Mungu kuchuma us changa likamtumikie Mbingun nasasa tumepata mwombez wetu mbingun ๐Ÿ™ nenda baba tutaonana badae

    ReplyDelete
  9. Hkweli Duniani tu wapitaji.Pumzika kwa Amani Baba.

    ReplyDelete
  10. Apumzike kwa Aman ni mapema sana ๐Ÿ˜ญ๐Ÿ˜ญ

    ReplyDelete
  11. Shairi nzuri lenye kusikitisha na huzuni kubwa pumzika kwa Amani padre

    ReplyDelete
  12. Aminaaa ๐Ÿ˜ญ๐Ÿ˜ญ pumzika kwa amani

    ReplyDelete
  13. Mungu ampe pumnziko la milele!

    ReplyDelete
  14. Mwenyez MUNGU amjalie pumziko la milele

    ReplyDelete
  15. Marehem apate rehema kwa mungu apumzike kwa amani๐Ÿ™๐Ÿ™

    ReplyDelete
  16. Dah ni mapema mnoo๐Ÿ˜ญ๐Ÿ˜ญ

    ReplyDelete
    Replies
    1. RIP amen ๐Ÿ™๐Ÿ™๐Ÿ™

      Delete
  17. Apumzike kwa Amani.

    ReplyDelete
  18. Kuna wakati wa kupanda na wakati wa kuvumuli

    ReplyDelete
  19. Blog ipo vizuri sana.tuendelee kuitumia,pia nimeona kipaji chako,kweli haubahatishi

    ReplyDelete
  20. RIP mpendwa wetu

    ReplyDelete

SMILE ON THE FACE; BUT...? by Fr. Joseph C. Ogbu

Imagine! Calmly water turning thicker than blood, Evils gently overflowing like flood. God! be merciful on your precious world, And allow n...